July 4, 2015


Taifa Stars imeng’olewa na michuano ya kuwania kucheza Kombe la Chan baada ya sare ya mabao 1-1 dhidi ya Uganda.

Katika mechi yao ya pili kwenye Uwanja wa Nakivubo jijini Kampala, leo Stars ilikomaa kwa sare ya bao 1-1.


Stars ilianza kupata bao kupitia John Bocco kwa mkwaju wa penalti kabla ya Uganda kusawazisha kupitia Telvon Kizito baada ya kumalizia kazi ya Robert Ssentongo.

Kwa sare hiyo Stars imeng'olewa kwa jumla ya mabao 4-1, hiyo ni baada ya kupoteza 3-0 mjini Zanzibar. Wakati huo timu ikiwa chini ya Mart Nooij ambaye ameishatupiwa virago.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic