July 13, 2015



Katika kuhakikisha kwamba kambi yao inakuwa na nidhamu ya hali ya juu pamoja na umoja, Kocha wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, alilazimika kubadilisha ratiba ya msosi wa jioni kambini hapo.

Simba ambayo imefikia kwenye hoteli ya Lushoto Executive, wachezaji walikuwa wakipata msosi kuanzia saa moja usiku tangu walipowasili hapo wiki moja nyuma.
KERR 
Baada ya kumalizika kwa mazoezi ya juzi Jumamosi, Kerr aliwaweka chini wachezaji hao na kuwaambia kwamba siku hiyo na inayofuatia, yaani jana Jumapili, watalazimika kula kwa pamoja saa 12:30 jioni ambapo lazima wote wakae pamoja kupata msosi huo wa usiku.

Kwa kawaida muda huo ni maalum kwa wachezaji waliofunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lakini kocha huyo akaona ni sahihi kujumuika nao ili kujenga umoja zaidi.

Lakini kiungo wa kikosi hicho, Mganda, Simon Sserunkuma, alionekana kutokubaliana na suala hilo na alihoji kama wakila muda huo je hawatakula tena usiku ambapo alikutana na jibu la Kerr lililosema ndiyo.

Kiungo huyo akaonekana kutokubaliana naye lakini aliamua kuacha kama ilivyo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic