Mashabiki mbalimbali wa
Simba wameonekana kutoelewa uuzwaji wa mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Mashabiki hao wametuma
ujumbe mfupi katika blog hii wakionyesha kutofurahishwa kutokana na kuuzwa kwa
Okwi.
Simba imemuuza Okwi
katika klabu ya Sonderjyske ya nchini Denmark lakini dau lake limeendelea kuwa siri
kubwa.
Wengi wao wameonyesha
kuwa jambo hilo limekuwa ni la kushitukiza na wanaona Mganda huyo alikuwa
msaada mkubwa katika kikosi chao.
“Inawezekana vipi,
wakati tunajiimarisha, halafu Okwi ndiyo anauzwa. Huyu ndiye alikuwa mchezaji
wetu aliyefanya vizuri msimu iliopita,” alisema Mohammed Said.
Thomas Maganga
aliyejitambulisha kuwa mmoja wa mashabiki wa kutupa wa Simba, alisema: “Naanza
kuona kama kuna shida, uuzwaji wa Okwi katika wakati huu kama tulikuwa tuna nia
ya kujenga kikosi naona si sahihi.”
Asilimia kubwa ya
mashabiki hao walionekana kuwa na hofu kuu. Hata hivyo, baadhi yao walisema si
jambo baya kumuuza.
“Unajua Okwi ni mzuri
lakini msumbufu, hivyo muache aende tu halafu tujipange.”
Kuhusiana na hilo,
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alilitolea
ufafanuzi na kusema.
“Wale watu tuliona ofa
yao ni nzuri,” alisema bila ya kuitaja.
“Ukiachana na hivyo,
Okwi na Simba kuna makubaliano katika mkataba, moja ni hilo suala kwamba
akipata timu tumuachie.
Sasa sioni kama kuna
tatizo na lazima mjue wachezaji wanakuja na kuondoka,” alisema Hans Poppe..
Tatizo sio kuondoka, bali kwanini hatutajiwi dau ameuzwa kiasi gani!! Muda wa kufanya hizi club shamba la bibi uishe jamani!!
ReplyDeleteMhh mie nimeanza kuwa na wasiwasi na Hans Pope....unauazaje machine kama Okwi na huku unasema tunataka ubingwa?....sielewi
ReplyDelete