July 7, 2015


Kiungo Ramadhani Singano ‘Messi’, sasa ni mchezaji huru.
Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji imechukua uamuzi wa kuvunja mkataba kati ya Messi na Simba.


Mwenyekiti wa kamati hiyo, Richard Sinamtwa amesema amevunja mkataba huo kwa kuwa Simba ilishindwa kutekeleza vipengele kadhaa vya mkataba.

“Tumefikia uamuzi wa kuvunja mkataba huo na sasa Messi ni mchezaji huru. Simba wameonekana kutekeleza vipengele.

“Mfano kuanzia bima kulikuwa na tatizo, lakini Simba walileta ushahidi kwamba walimlipia. Tukaingia katika suala la pango.
“Hapo kukawa na tatizo, Simba wameshindwa kuthibitisha hilo na kuonekana kuna tatizo,” alisema.

Awali kulikuwa na madai kwamba Simba wanasema wana mkataba wa miaka mitatu na Messi na yeye alisema ana mkataba wa miaka miwili tu.

“Hilo suala halikuletwa kwenye kamati yetu kwa kweli. Sisi ilikuwa ni uvunjwaji wa vipengele vya mikataba.


“Hivyo tusingeweza kujadili suala ambalo halikuletwa kwenye kamati,” alisema Sinamtwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic