July 12, 2015

 Beki wa amani wa Simba, Emily Mgeta amesema yuko tayari kupambana na changamoto za kisoka nchini Ujerumani.


Mgeta amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Neckarsulmer ya Ujerumani

Akizungumza na SALEHJEMBE, Mgeta amesema anaamini Ujeurmani kuna ushindani zaidi ya nyumbani Tanzania lakini anataka kutimiza ndoto yake.

“Watu wa hapa ni wapambanaji, najifunza mengi kupitia wao lakini sitakubali kushindwa. Nataka kufanya vizuri na kufikia ndoto zangu,” alisema.

Mgeta amewahi kuichezea Simba katika kipindi cha makocha wawilim tofauti, Patrick Liewig na Zdravko Logarusic.


Tayari ameanza mazoezi na kikosi chake hicho kipya kinachoshiriki Ligi Daraja la Tano akijifua kwa ajili ya msimu mpya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic