Baada
ya chenga nyingi, sasa mambo yako hadharani kuwa Simba imemuuza Emmanuel Okwi
kwa Sh milioni 220.
Okwi
ameuzwa katika klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark ambayo amejiunga nayo kwa mkataba wa miaka mitano.
Awali,
Simba kupitia kaimu katibu wake mkuu, Collins Frisch ilikuwa ikifanya siri
kubwa bila sababu yoyote.
Lakini
uongozi wa SønderjyskE umeweka wazi kwamba umemnunua Okwi kwa
dola 110,000.
Baadaye
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe naye
amelithibitisha hilo.
“Kweli
ni fedha hizo, katikati ya mwezi huu nafikiri tarehe 17, watatulipa,” alisema.
Tayari Okwi ameichezea timu hiyo kwa dakika 76 katika mechi
ya kirafiki dhidi ya Schleswigers.
0 COMMENTS:
Post a Comment