AMINA (KULIA) AKIWA NA RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI. |
Uchaguzi wa Chama cha Soka cha Wanawake Tanzania (TWFA)
umemalizika ambapo Amina Karuma amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa
chama hicho, kufuatia uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya katibu msaidizi imekwenda kwa mwandishi wa habari za
michezo Someo Ng’itu, na nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFWA
imekwenda kwa Debora Mkemwa na Theresia Mng’ongo.
Mgeni
rasmi katika uchaguzo huo alikuwa ni katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine ambapo
na uchaguzi ulisimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya uangalizi wa
Jeremia Wambura kutoka kamati ya Uchaguzi ya TFF.
TFF
inawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na kuwatakia kila la kheri katika
majukumu hayo mapya, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika maendeleo ya
mpira wa miguu ya wanawake nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment