August 19, 2015


Kikosi cha Azam FC, kimekuwa kikiendelea na mazoezi yake kimyakimya.


Azam FC inakutana na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Keshokutwa kukipiga katika mechi ya Ngao ya Jamii.

Tayari Azam FC imerejea Dar es Salaam kimyakimya na imeendelea kujifua kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, kimyakimya.

Azam FC inakutana na Yanga baada ya kushika nafasi ya pili msimu uliopita, pia imekuwa ni kawaida bingwa na mshindi wa pili kukutana kabla ya kufungua msimu.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema wamekuwa wakifanya mazoezi kama sehemu ya marekebisho na kuendelea kujiweka fiti.

"Baada ya mechi za kirafiki, kuna jambo jipya unajifunza. Kila siku lazima urekebishe jambo kwa kuwa soka ni mchezo wa mafunzo.

"Tunaendelea vizuri, kikosi kipo vizuri na tunaamini hadi siku ya mchezo tutakuwa vizuri," alisema Hall raia wa Uingereza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic