August 13, 2015

AKISAINI MBELE YA MANARA...

Mshambuliaji Mzimbabwe, Justice Majabvi amesajili mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba na kusema, anajiamini.


Majabvi amesema anaamini usajili wake Simba utakuwa na matunda kwa kuwa anaamini uwezo wake pia kikosi cha Simba.

“Simba ni timu bora kabisa, nimekaa siku chache hapa lakini nimeona kuna mengi ya kujifunza, pia ni kikosi chenye ushindani mkubwa kwa kuwa kimejaza wachezaji wenye vipaji.

“Ninaamini tutashirikiana vizuri na kuisaidia Simba, najiamini. Pia ninawaamini wenzangu,” alisema.


Mzimbabwe huyo alisaini mkataba wake huo mbele ya msemaji wa Simba, Haji Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic