August 13, 2015


Ingawa suala limekuwa likienda kwa siri kubwa lakini ukweli ni kwamba Kocha Dylan Kerr wa Simba ameishaeleza kutoridhishwa na kiwango cha Elius Maguri na yuko tayari aachwe.


Habari za ndani kutoka ndani ya Simba zimeeleza kocha huyo Mwingereza ameonyesha kutovutiwa na kiwango cha Maguri, hivyo ameuambia uongozi unaweza kumuonyesha mlango wa kutokea.

"Ni kweli, kocha ndiye amesema kwamba haridhishwi na Maguri. Amefanya naye kazi kwa zaidi ya mwezi sasa na anaona hafurahishwi naye.

"Kuhusiana na kumuacha kwenye kikosi ilikuwa ni siku ya Simba Day, lakini unaona Maguri kwa nini hakutambulishwa. Ilitakiwa atambulishwe kama wachezaji wengine, lakini akatolewa kabisa.

"Hapo utapata jibu kwamba Maguri hana chake Simba ingawa inaonekana anakosekana wa kumueleza ukweli," kilieleza chanzo.

Lakini leo mchana, Rais wa Simba, Evans Aveva amesema suala hilo limerudishwa kwenye kamati ya usajili.

"Kocha ndiye alitaka Maguri aondolewe kwenye kikosi siku ya Simba Day. Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau kwamba tunawaingilia makocha, hasa klabu hizi kubwa za Simba na Yanga.

"Sisi hatukutaka hilo litokee, tukampisha kocha afanye kazi yake," alisema Aveva.

"Lakini suala la Maguri liko kwenye kamati ya usajili, mnajua huyo ni mchezaji wetu kabisa," alisema Aveva.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic