August 13, 2015

NAFTALI (KUSHOTO) AKIMKABA OLUNGA ANAYEJARIBU MBINU KUMTOKA...
Unamkumbuka yule beki wa zamani wa Simba, David Naftali.
Jamaa fulani mkimya hivi na amepotea muda mrefu, lakini amefanikiwa kupasua na sasa anakipiga nchini Kenya.

Juzi ameonyesha uwezo mkubwa akiichezea timu ya mapato ya Kenya (KRA) kwa kumthibiti vilivyo mshambuliaji Michael Olunga wa Gor Mahia.

Naftali alimkamata Olunga vilivyo ingawa KRA ilifungwa kwa mabao 2-0, lakini Olunga hakufunga hata moja.

Hali hiyo ilimfanya Olunga kuwa na jazba, kwani hata mipira ya kichwa ilikuwa ni kazi kupiga kwa kuwa Naftali naye ni ‘mtu kweli’.


Olunga ndiye aliibuka mfungaji bora wa michuano ya Kagame ambayo Azam FC iliibuka bingwa bila ya kufungwa hata bao moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic