August 29, 2015


Na Saleh Ally, Kertepe
Baada ya mechi ya kirafiki dhidi ya Libya, Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema ataanza kuyafanyia kazi makosa ambayo ameyaona.

Baadhi ya makosa au matatizo wanayotakiwa kurekebisha ni pamoja na sehemu ya kiungo, pia ushambuliaji ikiwa ni pamoja na kutumia nafasi.

Akizungumza na Championi Jumamosi mjini hapa, Mkwasa alisema kuna mambo kadhaa ambayo wameyaona kama hilo la utengenezaji nafasi na umaliziaji.

“Katika soka makosa ni kila siku mnachofanya ni kujifunza. Utaona tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi kuliko Libya, lakini hatukuzitumia.

 “Lakini bado sijaridhika kutokana na utengenezaji pia, bado kuna mambo ya kurekebisha kwenye kiungo ambayo pia ni muhimu.

“Upande wa bao la kwanza umeona, lakini bao la pili pia lazima tuwe makini kwa kuwa kipa hakuwa makini. Bado hatuwezi kumuangushia mzigo, lakini tutatumia kosa lake kama sehemu ya kuwa makini zaidi,” alisema Mkwasa.


Stars itaendelea na mazoezi leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi yake kujifua kuiwinda Nigeria katika mechi itakayopigwa Septemba 5 jijini Dar es Salaam.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic