August 29, 2015


Siku ya leo ni maadhimisho ya Ndanda Day ambapo inatimiza miaka 14 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo, uongozi wa timu hiyo umesema kuwa sikukuu yao wataitumia kwa kuwatembelea wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Ligula iliyopo mkoani humo.

Ofisa habari wa timu hiyo, Idrisa Bandari alisema baada ya kuwatembelea wagonjwa jioni watajitupa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam FC.  

“Unajua neema huwa zinakuja kwa njia nyingi, kila jambo ambalo linampendeza Mungu huwa linaleta Baraka, hivyo katika maadhimisho ya Ndanda Day tutafanya mambo mawili tu, kuwatembelea wagonjwa pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na Azam.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic