August 7, 2015

MAVUGO, AMESHINDWA KUJIUNGA NA SIMBA...
Mshambuliaji Kelvin Ndayisenga raia wa Burundi ametua nchini  leo saa 1 usiku tayari kufanya majaribio katika kikosi cha Simba.



Simba imeendelea na harakati zake za kusaka mshambuliaji ikiwa ni siku chache baada ya kupata uhakika mshambuliaji Laudit Mavugo hatakuja nchini kujiunga na nayo.

Mrundi huyo anayetokea katika kikosi cha  AO Bujumbura ametua nchini na kujichimbia katika moja ya hoteli bora nchini ya Sapphire Garden Court.

Kwa mujibu wa uongozi wa Simba, Ndayisenga atakabidhiwa kwa Kocha Dylan Kerr raia wa Uingereza ambaye atakuwa na kazi ya kumhakiki mshambuliaji huyo.

“Kweli amewasili leo na jukumu atakabidhiwa kocha Kerr na benchi lake la ufundi kuamua kuwa wanamuonaje.


“Kwa sasa dirisha la usajili limesogezwa mbele, hivyo kinachofuata sasa ni suala la la kumalizia usajili,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic