MWENYEKITI WA KAMATI YA USAJILI YA SIMBA, ZACHARIA HANS POPPE |
Unaweza ukasema hii sasa sifa, maana Simba ndani
ya siku tatu itakuwa imeshusha wachezaji watatu wa kimataifa kwa ajili ya
majaribio.
Kwanza leo imeanza na Mshambuliaji Kelvin
Ndayisenga raia wa Burundi ambaye ametokea AO Bujumbura ya kwao Burundi na
anatarajia kuanza majaribio mara moja.
Lakini kesho alfajiri, kipa Ricardo Andrade
anatua nchi tayari kuanza majaribio. Kipa huyo raia wa Brazil alikuwa anakipiga
katika klabu ya Sporting ya nchini Ureno.
Wakati kipa huyo atakuwa amekamilisha idadi ya
wachezaji wawili wapya wa kigeni waliotua nchini ndani ya siku mbili, raia wa
Mali, atatua Jumatatu.
Huyo ni Makani
Dembele kutoka kutoka katika kikosi kikongwe cha JS Kabylie cha Algeria.
Rais wa Simba, Evans Aveva ameiambia SALEHJEMBE,
kwamba ni katika harakati zao za kuhakikisha wanajenga kikosi chao.
“Yote ni mikakati ya usajili, kamati ya usajili
kwa kushirikiana na benchi la ufundi pamoja na kamati ya utendaji, imekuwa
ikiendelea na kazi zake,” alisema Aveva.
Kesho ni siku muhimu kwa Simba, maarufu kama
Simba Day na mashabiki wa Simba watapata nafasi ya kuwaona wachezaji hao.
0 COMMENTS:
Post a Comment