Barcelona
imeonyesha kiwango na kuichapa AS Roma kwa mabao 3-0 katika mechi ya kirafiki
jana, lakini mshambuliaji wake Lionel Messi nusura alambwe kadi nyekundu.
Messi alinusurika
tu baada ya kumpiga kichwa kwa makusudi na kumkaba beki Mapou Yanga-Mbiwa walipokuwa
wanazozana. Wote wawili walilambwa kadi nyekundu.
Bao la kwanza
lilifungwa na Neymar kabla ya Messi na Raktic kuimalizia kazi ya tatu bila.
0 COMMENTS:
Post a Comment