BOSSOU... |
Beki wa kati wa timu ya
taifa ya Togo, Vicent Bossou ametua nchini leo alfajiri tayari kujiunga na
Yanga.
Bossou ni tegemeo katika kikosi cha Togo kinachoongozwa na nahodha Emmanuel Adebayor na kufundisha na kocha wa zamani wa Yanga, Tom Saintfiet.
Beki huyo wa kati
ametua nchini siku moja baada ya Mzimbabwe, Thaban Kamusoko ambaye alikuwa
akikipiga FC Platinum pamoja na mshambuliaji wa sasa wa Yanga, Donald Ngoma.
Timu ya mwisho ya
Bossou inaonekana kuwa ni Goyang Hi FC ya nchini Korea na leo ametua nchini
kufanya mazungumzo ya mwisho na Yanga.
Beki huyo ambaye pia
aliwahi kukipiga Etoile du Sahel ya Tunisia anajiunga na Yanga kwa ajili aya
kuimarisha safu ya ulinzi ambayo inaonekana kuyumba.
Yanga imemsajili
Kamusoko kwa ajili ya kuyumba kwa safu yake ya kiungo cha ukabaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment