August 16, 2015


Yanga imeitwanga Mbeya City kwa kuichapa kwa mabao 3-2 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.


Yanga ambayo imepiga kambi Tukuyu ilionyesha soka safi na kuibana Mbeya City iliyokuwa nyumbani.

Mabao ya Yanga yalitupiwa kambani na wageni tu, alianza Andre Coutinho raia wa Brazil.

Baada ya hapo, Amissi Tambwe akatupia la pili kabla ya Donald Ngoma raia wa Zimbabwe kupiga la tatu.

Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Bakari Slang na Joseph Mahundi aliyefunga katika dakika ya 90.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic