August 18, 2015

Kipa mkongwe  aliyeachwa Simba, Ivo Mapunda amesema suala la kwamba hakutoa ushirikiano ni propaganda tu za viongozi.


Ivo Mapunda amesema sababu ya Simba kutompa mkataba mpya kwa madai hakutoa ushirikiano, hazina mashiko.


Kipa huyo mkongwe, amechwa na Simba ambayo tayari ilishampa Sh milioni 8 kwa ajili ya usajili.

“Kwa kweli ni propaganda tu za viongozi. Mimi hilo haliniingii akilini kwamba sikutoa ushirikiano.

“Nilikuwepo, baadhi ya viongozi tulikuwa tukiwasiliana wakati nikipatiwa matibabu. Sasa sijui hilo linatolea wapi,” alisema Mapunda ambaye kabla ya kutua Simba alikuwa Gor Mahia.


Simba imeamuacha Ivo na kuzua mjadala mkubwa lakini benchi la ufundi linaonekana kuridhika na kipa mpya raia wa Ivory Coast.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic