Kocha wa Mwadui FC ya mkoani Shinyanga, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ameamua kujichimbia
mafichoni na timu yake kabla ya
kuanza msimu mpya ili kuhakikisha
anafanikiwa kuwa na ushindani mkubwa msimu ujao.
Mwadui FC imepanda daraja msimu uliopita ikiwa ni miongoni mwa
timu nne zilizopanda daraja, zikiwemo Majimaji ya Songea, African Sport ya
Tanga na Toto Africans ya jijini Mwanza.
Julio amesema kuwa ameamua kukificha kikosi chake kuhakikisha kinaiva
kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu.
“Kwa sasa tupo mafichoni tukiwa katika ‘Pre Sesons’ kabla ya
kuanza kwa msimu mpya, nikiwa nawapatia mazoezi mazito wachezaji wangu,
hatutaki mtu yeyote ajue.
“Tunajiandaa kwa ajili ya kuweka kambi nje ya nchi hata muda wa
siku 10 na mambo yakikamilika, tutatoa taarifa juu ya nini tunakifanya,
tutacheza mechi za kirafiki hapo baadaye lakini kwa sasa bado tunaendelea na
mazoezi kwanza,” alisema Julio.
0 COMMENTS:
Post a Comment