Kipa Petr Cech aliyeonekana shujaa mpya wa Arsenal baada ya mechi
ya Ngao ya Jamii dhidi ya Chelsea, sasa amegeuka adui.
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal walionyesha bango linalomshukuru
kipa huyo wa zamani wa Chelsea, lakini pia linamsisitiza aondoke zake.
Katika bango hilo, mashabiki hao wa Arsenal wanaona sasa ndiyo
wakati mwafaka wa Cech kuondoka Arsenal.
Lakini inashangaza kwa kuwa ameichezea Arsenal mechi moja tu ya
ligi ambayo Arsenal ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya West Ham.
Kipigo hicho kimezua mjadala na Cech anaonekana alicheza chini ya
kiwango na kusababisha Arsenal kufungwa mabao yote mawili.
0 COMMENTS:
Post a Comment