Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu
ameanza kampeni ya waziwazi kwamba wachezaji wake watatu ndiyo wana nafasi ya
kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia.
Tuzo hiyo maarufu kama FIFA Ballon d'Or, sasa
inashikiliwa na mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Josep amesema Lionel Messi anayepewa naafsi
kubwa ya kuibeba, Luis Suarez na Neymar ndiyo wanaostahili.
Wachezaji hao wa Barcelona wote wanatokea katika bara la Amerika Kusini katika nchi za Argentina, Urugauay na Brazil.
Maneno ya Rais huyo wa Barcelona yanaonekana ni
kama kampeni za mapema na makusudi.
Kama watatu hao wataingia fainali, halafu Messi
akashinda, inakuwa ni sifa kubwa kwa Barcelona ambayo kibiashara ni msaada
mkubwa kwa klabu hiyo kama ambavyo waliwahi kufanya Xavi, Iniesta na Messi.
0 COMMENTS:
Post a Comment