August 17, 2015


Kampuni kubwa ya matairi ya Lassa ya Uturuki, imeingia mkataba wa matangazo na kiungo mpya wa Barcelona, Arda Turan.

Turan raia wa Uturuki na naodha wa timu ya taifa, amejiunga na Barcelona akitokea Atletico Madrid.

Lassa imeingia mkataba wa miaka minne na Turan, sawa na ilivyo kwa Barcelona ambayo pia imeingia mkataba wa muda huo na kampuni hiyo ya kuuza na kutengeneza matairi.

Kwa hapa nyumbani tanzania, kampuni ya maarufu ya matairi inayojihusisha na michezo zaidi ni ile ya Bin Slum ya jijini Dar es Salaam.

Misimu mitatu iliyopita, kampuni hiyo iliidhamini Coastal Union hadi iliporejea Ligi Kuu Bara.


Lakini msimu uliopita, ikaweka rekodi nyingine ya kudhamini timu tatu changa ambazo ni Mbeya City, Ndanda FC pamoja na Stand United.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic