Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
ambaye amekatwa kuwania udiwani Mbagala Kuu, amesema alikuwa ni mgonjwa.
Manji ambaye ameshinda kwa kura nyingi
katika kura za maoni, lakini akaenguliwa kwa madai hakuwa katika eneo husika,
imesababisha kuzua hasira kwa wananchi wa eneo hilo.
Jana wananchi hao walifika katika
Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam wakitaka kujua hatma ya Manji.
Wengi walihoji kwamba Manji amekatwa
kwa fitna zinazozihusisha Yanga na Simba ambazo ni klabu kongwe za soka nchini.
“Nilikuwa mgonjwa, inajulikana. Hali yangu
haikuwa nzuri, hivyo nisingeweza kufika,” alisema Manji alipozungumza na
SALEHJEMBE.
Hata hivyo Manji alisisitiza,
asingependa kulizungumzia suala hilo kwa kuwa bado linasikilizwa ndani ya
chama.
“Nafikiri tuache kwanza, subira ni
jambo zuri sana,” alisema Manji.
0 COMMENTS:
Post a Comment