August 7, 2015


Baada ya Toto Africans ya jijini hapa kumpata kocha mpya kutoka nchini Ujerumani, Martine Grelics, kocha huyo amefunguka na kusema kuwa hatishwi na uwezo wa timu za Simba, Yanga na Azam FC na kudai kuwa lengo yake ni kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara.


Akizungumza ikiwa ni siku ya pili tangu kutua nchini, Grelics alisema amekuja kufanya mabadiliko ndani ya kikosi cha Toto kwa kuwafundisha falsafa mpya.

“Imani yangu ni kwamba endapo wachezaji watanielewa basi Toto itakuwa tishio. Nimesikia uwepo wa timu kubwa hapa nchini kama Yanga, Simba na Azam, hivyo nitakiandaa kikosi changu ili kiweze kuwa mfano wa kuigwa kwa kuhakikisha kuwa timu inapata matokeo yatakayoifanya ipate nafasi muhimu katika ligi,” alisema na kuongeza:


“Muda siyo mrefu tutaanza mazoezi magumu ambayo yatasaidia wachezaji kwa jumla kuwa fiti na kuwa na nguvu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic