August 8, 2015


Leo ndiyo Simba Day na Simba inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya SC Villa ya Uganda katika maadhimisho ya Tamasha la Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa Dar, straika wa timu hiyo Mussa Mgosi amesema wamejipanga kutowaangusha mashabiki wao.

Mgosi amesema kwa kambi mbili walizopiga Lushoto, Tanga na Zanzibar hivi karibuni kikosi chao kimebadilika na sasa kina uwezo wa kuitetemesha timu yoyote.

Mgosi alisema atahakikisha anashirikiana vizuri na wenzake ili Simba ishinde kufuta dhana ya kufanya vibaya katika mechi za timu hiyo katika Simba Day.

“Binafsi naona maandalizi yameenda vizuri kuanzia katika kambi ya Lushoto na hata Zanzibar kwa sababu tumecheza mechi za kirafiki za kutosha, naamini kuwa zimetujenga vya kutosha,” alisema Mgosi.


“Nawaomba mashabiki waje kwa wingi kuiangalia timu yao maana tunafahamu kuwa ni kipindi kirefu hawajaiona na haitakuwa vizuri tukipoteza mbele yao, hivyo tutapambana ili tushinde.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic