August 8, 2015


Kiungo ‘rasta’, Thabani Kamusoko yupo katika hatua za kusaini mkataba wa kuichezea Yanga akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, amewaambia mashabiki wa timu hiyo kuwa amekuja kufanya kazi na siyo masihara.


Kamusoko raia wa Zimbabwe jana Ijumaa alifanya mazoezi kwa mara ya kwanza na Yanga kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam chini ya uangalizi wa Kocha Hans van Der Pluijm na Katibu Mkuu, Dk Jonas Tiboroha. 

Katika mazoezi hayo, Kamusoko alionekana kufanya vizuri katika mazoezi ya kukaba na kupiga mipira mirefu kwa washambuliaji na mashuti makali kuelekea lango la adui.

Kamusoko alisema: “Naijua vizuri Yanga tangu mwaka 2002, ni timu nzuri yenye wachezaji wenye ushindani, nitapambana kuhakikisha napata nafasi ya kucheza.

“Nimekuja Tanzania kufanya kazi, nataka mashabiki wajue hivyo na wasidhani nimekuja kufanya mambo mengine hapa, nipo kazini.”alisema Kamusoko’’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic