MKUU WA KITENGO CHA HABARI CHA DRFA, OMARY KATANGA (KUSHOTO) AKIWA NA VIONGOZI WENGINE WA CHAMA HICHO. KATIKATI NI BENNY KISAKA.
MAAMUZI YA KAMATI YA UCHAGUZI YA DRFA
KUHUSU RUFANI ZA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI WA CHAMA
CHA SOKA WILAYA YA TEMEKE (TEFA) KUPINGA MAAMUZI YA KAMATI YA UCHAGUZI YA
TEFA. ZILIZOSIKILIZWA TAREHE 10/08/2015
KATIKA HOTELI YA PR TEMEKE.
WAJUMBE WALIOHUDHURIA NI:
1. RASHID
SAADALLAH-MWENYEKITI
2. FAHAD
F.A. KAYUGA-KATIBU
3. JUMA
PINTO-MJUMBE
4. HAJI
BECHINA-MJUMBE
1. RASHID SALIM-NAFASI
YA MWENYEKITI WA TEFA
-Kashindwa
kuleta vielelezo kuthibitisha uzoefu wake katika masuala ya mpira kama Ibara ya
31(1)(j) inavyosema, alidai kuwa amekuwa kiongozi wa Tandika FC kwa
muda wa miaka saba lakini hukuweza kuthibitisha maelezo yake kwa vielelezo. Kwa
hivyo kamati inakubaliana na maamuzi ya kumuengua ya kamati ya uchaguzi TEFA.
2. PETER STEPHEN MUHUNZI-NAFASI YA
MWENYEKITI WA TEFA
-Kathibitisha kigezo cha elimu kwa maana
ya kumaliza kidato cha nne ingawa kuna pingamizi la matumizi mabaya ya fedha na
ubadhirifu, haya kamati yangu haina mamlaka ya kuyatolea maamuzi hivyo
yanapelekwa kwenye kamati ya maadili ya DRFA.
3. AZIZ MOHAMED
KHALFAN-NAFASI YA MWENYEKITI WA TEFA
-kamati
imegundua kwamba alienda kwenye mchakato wa uchaguzi akiwa hana sifa kwa sababu
alifungiwa na kamati ya nidhamu na usuluhishi ya kutokushiriki au kujihusisha
na mpira kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) na TEFA hata hivyo hakukata rufaa
juu ya kifungo hicho na badala yake alikwenda kupeleka malalamiko yake TFF.
Kiutaratibu baada ya kufungiwa na kamati tajwa alipaswa akate rufaa katika
kamati ya rufaa ya TEFA, na kama asingeridhika na maamuzi ya kamati ya rufaa ya
TEFA ndiyo angeweza kukata rufaa katika kamati ya uchaguzi ya DRFA. Kwa maana
hiyo kamati inamuengua kwa sababu rufaa yake imeshindwa kuzingatia kanuni na
taratibu za kukata rufaa.
4. SIZZA CHENJA-NAFASI YA MWENYEKITI WA
TEFA
-kamati imempitisha aendelee na mchakato
wa uchaguzi baada ya kuthibitisha kuwa ana uzoefu wa kutosha katika uongozi wa
mpira wa miguu kama katiba ya TEFA Ibara ya (31)(1)(j) inavyotaka. Kwani mnamo
mwaka 2009 alikua kiongozi katika klabu ya soka ya Tp Vita vilevile ameweza
kushiriki ugombea katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wa DRFA katika
vipindi tofauti ikiwemo mwaka 2012 ambapo alishindwa kupata nafasi hiyo.
5. OMARY. A. KAPILIMA-NAFASI YA MAKAMU YA
KWANZA WA MWENYEKITI
-kaweza kuthibitisha uzoefu wa uongozi wa
mpira lakini kashindwa kuleta cheti cha kidato cha nne kinachotambulika na
Baraza la Mitihani la Taifa yaani (NECTA). Hivyo maamuzi ni kuwa kashindwa
kukidhi kigezo cha elimu kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya
TEFA.
6. SALEHE MOHAMED SALEHE-NAFASI YA MAKAMU
WA KWANZA WA MWENYEKITI
Kamati inamuengua katika mchakato wa
uchaguzi kwa kushindwa kuthibitisha kiwango chake cha elimu kwa kushindwa
kuleta cheti cha kidato cha nne(Academic Certificate) kama inavyotakiwa na
Ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA. Pia kulikuwa na madai ya
ubadhirifu wa fedha na kuuza timu ya Tesema FC akiwa kama makamu wa kwanza wa
mwenyekiti wa TEFA, haya kamati inayapeleka katika kamati ya maadili ya DRFA
kwa ufafanuzi na maamuzi.
7. SHUFAA JUMANNE- NAFASI YA MAKAMU WA
KWANZA WA MWENYEKITI
-Kamati inampitisha aendelee na mchakato
wa uchaguzi baada ya kuridhika na uthibitisho wa uzoefu wa zaidi ya miaka
mitatu katika uongozi wa soka. Ameweza kuithibitishia kamati kwa
vielelezo kuwa amekuwa kiongozi wa Tale FC kwa zaidi ya miaka mitatu. Vilevile
ameleta vielelezo kuthibitisha kuwa Tale FC ni mwanachama hai wa TEFA kinyume
na madai ya mpingaji.
8. DAUDI FRANCIS MUMBULI-NAFASI YA MAKAMU
WA KWANZA WA MWENYEKITI
-Kamati
inaitupilia mbali rufani hii baada muweka pingamizi kushindwa kutokea mbele ya
kamati kuthibitisha madai yake. Hivyo maamuzi ya kamati ya uchaguzi y a TEFA
yanabaki kama yalivyo. .
9. BAKILI M. MAKELE-NAFASI YA MAKAMU WA
PILI WA MWENYEKITI
-Kamati imemuengua katika mchakato wa
uchaguzi kwa kigezo cha elimu, kama inavyotakiwa na Ibara ya 31(1)(b) ya katiba
ya TEFA . Mgombea amekiri kwamba elimu yake ni ya darasa la saba.
10. AMACK NABOLA- NAFASI YA UJUMBE SOKA LA
WANAWAKE NA VIJANA
-Kamati
inamuengua katika mchakato kwa kukosa sifa ya elimu ya kidato cha nne kama
ibara ya 31(1)(b) ya katiba ya TEFA inavyotaka. Amack Nabola anagombea nafasi
ya ujumbe wa soka la wanawake na vijana hivyo halindwi na ibara ndogo katika
ibara ya 31 ambayo inatoa sifa za mgombea nafasi ya ujumbe wa kamati ya
utendaji kwa kumtaka mjumbe awe na elimu isiyo chini ya darasa la
saba. Ibara hii ipo kwa ajili ya wagombea wanaogombea nafasi za
ujumbe wa kamati ya utendaji na si wajumbe wa makundi mbali mbali kama vile
kundi la wanawake na vijana.
11. FIKIRI MAGOSO-NAFASI NI MJUMBE WA
KAMATI YA UTENDAJI
-Kamati
inampitisha kugombea nafasi hii kwa sababu anakidhi vigezo kwa kuwa na cheti
cha darasa la saba kama katiba ya TEFA anavyomtaka mgombea wa nafasi ya ujumbe
wa kamati ya utendaji kuwa na elimu isiyo chini ya darasa la saba.
12. MUHIBU KANU MSHANGAMA- MAKAMU
MWENYEKITI NA MJUMBE KAMATI YA UTENDAJI.
- Kamati
inamuengua kwa sababu ni kinyume cha kanuni za uchaguzi za TFF za
mwaka 2013 (TFF ELECTORAL CODE) Ibara 10(9) ambayo inakataza mgombea kugombea
nafasi zaidi ya moja. Muhibu Kanu Mshangama anagombea nafasi ya makamu mwenyeki
wa pili na mjumbe wa kamati ya utendaji kupitia kanda tandika.
MWENYEKITI
RASHID SADALA (ADVOCATE)
0 COMMENTS:
Post a Comment