MAKAPU (KUSHOTO) AKIPAMBANA NA AJIBU |
Siku chache baada ya Yanga kutolewa katika
michuano ya Kombe la Kagame, kiungo mkabaji wa timu hiyo, Saidi Juma Makapu,
amesema amehuzunishwa na taarifa za watu kusema safu ya kiungo mkabaji ndiyo
iliyokuwa tatizo katika kikosi hicho, badala yake amesisitiza Yanga ilitolewa
kama timu na si tatizo la mtu mmoja.
Licha ya Yanga kupewa nafasi kubwa ya kufika
fainali, iliondolewa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na Azam kwa mikwaju
ya penalti 5-3, huku beki wa timu hiyo, Haji Mwinyi Mngwali akipoteza mkwaju
wake.
Makapu hakucheza michuano hiyo kutokana na
majeraha.
“Nimeumia sana kusema kwamba kiungo cha Yanga
kilipwaya katika Kagame, sisi tunacheza kama timu na siyo mtu mmoja. Kwangu
namuona Mbuyu Twite kama mtu aliyekuwa akicheza kwa juhudi uwanjani. Angalia ile
mechi na Wasudani (Al Khartoum), alicheza vizuri sana.
TWITE... |
“Cha muhimu ni kuchukua hilo kama funzo kwa
ajili ya kujiandaa na ligi na michuano ya kimataifa. Naamini urejeo wangu na
kwa kushirikiana na wenzangu, utakuwa na faida katika timu yetu,” alisema
Makapu.
Kwa mujibu wa Daktari wa Yanga, Juma
Sufiani, kiungo huyo anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wake
leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment