Mshambuliaji Laudit Mavugo amesema alikuwa tayari kujiunga Simba
kwa moyo safi lakini kutoelewana kwa viongozi wa pande mbili, ndiyo
kumesababisha.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Mavugo amesema kulitokea tofauti ndogo
ndogo sana kati ya viongozi wa timu yake ya Vital’O na Simba.
Amesema alishamalizana na Simba kwa maana ya makubaliano, ndiyo
maana alichukua hadi baadhi ya fedha lakini waliposhindana wenyewe, hakuwa na
ujanja.
“Kitu cha kwanza kilikuwa ni kuhusiana na fedha wanazodai
kuhusiana na uhamisho wa Amissi Tambwe ambazo hawajalipwa hadi leo.
“Pili viongozi wa Vital’O waliona Simba kama hawana ushirikiano na
wana dharau, hmaana waliwaomba mechi ya kirafiki, hawakujibu wala kujali
lolote,” alisema Mavugo.
0 COMMENTS:
Post a Comment