August 10, 2015

Mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo alitoa kali ya mwaka baada ya kuingia mtaani akiwa katika mavazi yaliyomuonyesha kama mtito wa mtu anayeishi mtaani.

Ronaldo alifanya hivyo katikati ya jiji la Madrid, alitumia muda mwingi akipiga danadana akitumia mpira huku watu wakimpita hata bila ya kumjali.
 
Wakati Fulani alimuona mrembo mmoja, haraka alimkimbilia na kumuomba namba ya simu, lakini mwanadada huyo akamtolea nje.

Baada ya kutoa ndevu na nywele bandia alizokuwa amebandika, watu walianza kumsogelea wengi wakitaka kumsalimia na kumshika tofauti na ule mwonekano wake wa awali kama mtu asiye na makazi.

Wakati anatoa ndevu na nywele bandia, Ronaldo alimzawadia mpira mtoto aliyeonekana kumfuatilia akifurahishwa na aina ya danadana za kiufundi alizokuwa akipiga licha ya kwamba hakujua ni Ronaldo.




WATU WAMESHITUKIA KUWA KUMBE HUYU NI RONALDO...

WAKATI AKIANDALIWA KABLA YA KUINGIA MTAANI...





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic