HAPA ALIAMUA KUJIFUA NA TIMU YA RUGBY ILI KUJIWEKA FITI ZAIDI. |
Mtanzania Emily
Mgeta sasa anajiandaa kuendelea kupasua anga katika soka la Ujerumani akiwa na
kikosi chake cha Neckarsulmer.
Neckarsulmer inashiriki daraja la tano na Mgeta anaonekana taratibu kujihakikishia
namba katika kikosi cha kwanza na wikiendi hii wanatarajia kucheza dhidi ya Schwäbisch Hall.
“Kweli tutacheza
na Schwabisch Hall, mechi itakuwa ngumu kwa kuwa jamaa ni wazuri lakini
tumepania kuendelea kufanya vema.
“Mazingira ya kazi
hapa ni mazuri lakini yanataka umakini na kujituma sana kaka. Naendelea
kujitahidi nifanye vizuri zaidi,”
alisema.
Mgeta aliwahi
kuichezea Simba pia Polisi Moro kabla ya kuondoka Tanzania na kujiunga na Neckarsulmer
.
Mgeta amesema anaamini kufanya vema kutamsaidia
kusonga mbele kimataifa, hivyo hatachoka.
0 COMMENTS:
Post a Comment