August 12, 2015


Kiungo mkabaji mpya wa Azam FC, Mnyarwanda, Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ ametamka kuwa hataki kutoka kwenye kikosi cha kwanza cha Muingereza, Stewart Hall kinachojiandaa na Ligi Kuu Bara.

Migi alipata ujasiri wa kuongea kauli hiyo baada ya kucheza mechi zote za Kagame akicheza namba sita inayochezwa na Muivory Coast, Kipre Balou na Mudathiri Yahaya.

Kiungo huyo anayetumia mguu wa kushoto, alitua nchini hivi karibuni akisaini mkataba wa miaka miwili.
Migi alisema kuwa kikubwa amejipanga kupambana ili kuhakikisha anaendelea kuwepo kwenye kikosi cha kwanza.

Migi alisema, upo ushindani mkubwa wa namba kwenye timu hiyo, hivyo pale mchezaji unapopata nafasi ya kucheza ni lazima ucheze kwa kujituma ili kocha akuamini aendelee kukupanga kikosini.

 “Nisingependa kuwazungumzia sana wachezaji ninaocheza nao nafasi moja uwanjani, lakini kwa kifupi tu, mimi nimepanga kuendelea kuwepo kwenye kikosi labda litokee tatizo la majeruhi pekee lakini siyo uwezo.


“Kikubwa ninashukuru kupewa nafasi ya kuaminika kwenye timu na kuingizwa kwenye kikosi cha kwanza moja kwa moja mara baada ya kujiunga na Azam tukishiriki Kombe la Kagame,” alisema Migi anayeichezea timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic