Simba
imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya KMKM ya Zanzibar.
Mechi hiyo
imepigwa leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar na KMKM ndiyo ilitangulia
kushinda.
Matheo
Anthony ‘rasta’ ndiye alitangulia kuifungia KMKM katika dakika ya 25 na 35
lakini baadaye Msimbazi wakaanza kurudisha majibu.
Hamisi Kiiza
aliisawazishia Simba katika dakika ya 41, hivyo timu zikaenda mapumziko KMKM 2,
Simba 1.
Kipindi cha
pili, vijana wa Dylan Kerr walionekana kucheza kwa kasi zaidi na kufanikiwa kupata
bao la pili katika dakika ya 74, Ibra ‘Cadabra’ Ajibu akifunga baada ya
kuunganisha pasi safi ya Mwalyanzi.
Wakati KMKM
wanajiuliza imekuwaje, Ajibu tena aliipatia Simba bao la tatu katika dakika ya
77 akiunganisha krosi safi ya Mwinyi Kazimoto aliyekuwa ameingia kuchukua
nafasi ya Kiiza.
Simba
imeendelea kuchukua ushindi katika mechi zake zote za kirafiki za hapa
Zanzibar.
0 COMMENTS:
Post a Comment