August 14, 2015

KIKOSI CHA NDANDA MSIMU ULIOPITA...

Wakati dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa wiki ijayo, Ndanda FC ya Mtwara ipo katika mazungumzo na kiungo mshambuliaji, Oziri Desmond, raia wa Nigeria, aliyeletwa nchini na mmoja wa viongozi wa Yanga SC.

Mchezaji huyo mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, anafanya majaribio na Ndanda FC chini ya Kocha Ngawina Ngawina na kama ataliridhisha benchi la ufundi la timu hiyo, atafanikiwa kusaini mkataba.


Desmond ameliambia gazeti hii kuwa, mchezaji huyo ameunganishwa kuja nchini kwa msaada wa Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, baada ya kukutana naye katika mitandao ya kijamii.

“Ninapenda mazingira ya Tanzania, ingawa nina muda mfupi tangu nifike hapa. Awali sikuwa nikifahamu chochote kuhusu hapa, lakini ninamshukuru Hafidh Saleh wa Yanga ndiye aliyenisaidia.

“Aliniambia atanipeleka Mbeya City lakini ilishindikana, ingawa sifahamu nini kilikwamisha, ndipo akaamua kunileta huku (Ndanda) ambapo napo wamenipokea vizuri, nina uhakika nitapata nafasi.

“Saleh nilikutana naye katika mitandao, akaniambia nimtumie video zangu, nikafanya hivyo ndiyo akanifanyia mpango,” alisema Mnigeria huyo.


Kabla ya kutua Ndanda, Mnigeria huyo amesema alicheza katika timu za Doan FC na Mayzz FC, zote za Yemen, pamoja na Mighty Blackpad ya Sierra Leone.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic