August 8, 2015


Uongozi wa Simba, umewataka mashabiki na wanachama wao kujitokeza kwa wingi katika siku yao maarufu kama Simba Day.

Simba Day inaadhimishwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kutakuwa na burudani mbalimbali kabla ya kikosi cha Simba kukipiga na wageni wake, SC Villa ya Uganda maarufu kama Jogoo.

Pamoja na burudani, watakaohudhuria uwanjani hapo watapata nafasi ya kutambulishwa kwa wchezaji wa kikosi cha Simba pamoja na benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Dylan Kerr raia wa Uingereza akisaidiana na Mtanzania, Selemani Matola.


Akizungumza na SALEHJEMBE, Evans Aveva amesema anawaomba mashabiki, wanachama wa Simba pamoja na wapenda michezo, kujitokeza kwa wingi.

“Nianze kwa kusema ninawakaribisha kwenye Simba Day, ni siku ya Simba ambayo ina historia yake. Tuungane kuisherekea, pia tunawakaribisha wapenda michezo wengine.

“Simba ni nembo ya michezo Tanzania na Afrika nzima, ndiyo maana tumekuwa wa kwanza kuanzisha Simba Day. Tunajua na timu nyingine wamekuwa na siku kama hii baada ya kufuata mfano wa Simba.

“Tujitokeze kwa wingi kuwaonyesha sisi ni wakongwe na wana mengi ya kuiga kwetu inapofikia siku kama hii,” alisema Aveva akionyesha kujiamini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic