August 6, 2015


Mshambuliaji wa Simba, Elius Maguri ameingia kwenye hofu kubwa ya kutemwa.
Taarifa za ndani ya Simba zimeeleza uongozi wa Simba umeamua kumtema.

Lakini taarifa nyingine zimeeleza kwamba Simba iko tayari kumtoa mkopo na imeishazitaarifu baadhi ya timu zinazomtaka.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Maguri amesema bado hajapewa taarifa rasmi na uongozi wa Simba, lakini dalili ya mvua ni mawingu.

“Nimeondolewa kwenye kambi kwa kwa ajili ya Simba Day.
“Kidogo imenishangaza kwa kuwa ni siku ambayo wachezaji wanapaswa kutambulishwa kwa wanachama na mashabiki.

“Kama sitambulishwi siku hiyo, maana yake siko kwenye hesabu za klabu. Lakini hakuna kiongozi aliyeniambia.

“Inaniumiza sana, hasa ukizingatia nimeachwa siku ya mwisho baada ya kufanya mazoezi kwa kujituma sana Zanzibar.


“Ajabu kuna timu ikiwemo Ndanda ya Mtwara zinanipigia zikitaka nijiunge nazo kwa kuwa uongozi wa Simba umezieleza kuwa zinichukue,” alisema Maguri akionekana kusononeka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic