August 8, 2015


Simba SC, leo inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya SC Villa ya Uganda kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam lakini kocha wake, Dylan Kerr amesema kikosi chake kipo vizuri na kitashinda mechi hiyo kutokana na rekodi yao.


Kerr ameliambia Championi Jumamosi kuwa, akiwa kambini Zanzibar wachezaji wake walionyesha uwezo mkubwa kiasi cha kuweza kufunga mabao 17 katika mechi tano ambazo huchukua dakika 450 huku ikifungwa mabao matatu tu.
Simba iliifuga Polisi ya Zanzibar mabao 4-0 kisha ikashinda mabao 4-0 dhidi ya Jang’ombe Boys, mabao 2-1 dhidi ya Kombaini ya Zanzibar pia ikaifunga KMKM mabao 3-2 na ikaifunga Black Sailor mabao 4-0.

“Unaiona hiyo rekodi? Tupo vizuri kwani wakati naichukua timu ilikuwa na matatizo kadhaa na sasa mambo yamebadilika na kila mchezaji ana hamu ya kupata ushindi.

“Mashabiki wajue kitu kimoja, sikuandaa kikosi changu kwa ajili ya mechi hii tu, bali na mechi nyingine ambazo tutakutana nazo katika ligi na matokeo tuliyoanza nayo Zanzibar nataka yaendelee katika mechi zote.”

Kerr raia wa Uingereza alisema sasa timu yake inacheza soka la kasi huku wakitumia pasi fupifupi kuelekea lango la adui na kila mchezaji anapata nafasi ya kucheza.soka.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic