Hi
Miaka 35 iliopita nikiwa na umri mdogo sana. Wakati
huo nikisoma nursery kwenye skuli ya Tanganyika... Nna kumbukumbu ya nusunusu
juu ya pengine mchezo wangu rasmi wa kwanza kushuhudia wa timu ya taifa ya
Tanzania ambayo ilikuwa ikicheza na nchi ya Nigeria (Green Eagle's).
Nimeita kumbukumbu
nusunusu sababu ya umri mdogo niliokuwa nao wakati huo. Lakini ktk nusu nnazozikumbuka.
Nilipanda basi la timu ya taifa ambalo kama sikosei those dayz FAT (sasa tff) walikuwa
wanalimiliki.
STARS INAENDELEA KUJIFUA NCHINI UTURUKI |
Nakumbuka timu iliondokea hoteli ya Africana na sisi tulikuwa
kule for weekend na mzee ambaye inawezekana alinipigia pande kupanda basi la
mashujaa wale ambao kwangu sitawasahau kamwe.
Nnazo kumbukumbu pia
bendi ya DDC Mlimani Park ilitumbuiza kabla na wakati wa mapumziko katika mechi
ile murua kabisa. Ingawa kwa siku zile sikujua kama wale ndio sikinde ngoma ya
ukae!
Nusunusu yangu
inanikumbusha kikosi kilichoanza game ile.
1-Juma Pondamali
2-Leopard Tasso Mukebezi
3-Hasan Zito Kiaratu
4-Jellah Mtagwa(C)
5-Ishaka Hassan Chukwu
6-Salim Amiri
7-Omari Hussein
8-Mohammed Rishard Adolph
9-Peter Tino
10-Mohammed Salum
11-Thuweni Ally
Kocha Mkuu alikuwa
Joel Nkaya Bendera,
kwangu hii timu ambayo
ilitoka kucheza fainali za mashindano ya Mataifa huru ya Afrika (Afcon) ilikuwa
timu bora ya taifa kuwahi kuiona ingawa nilikuwa nusu mtu!
Timu hii ilimkosa
nahodha wake mkuu Leodgar Chillah Tenga ambaye alikuwa ameumia kwenye
mchezo wa liliokuwa kombe maarufu siku
hzo likiitwa Jengo Cup ambapo timu yake ya pan African ilicheza na yanga.
Bahati mbaya hyo ndiyo
ilikuwa game ya mwisho rasmi kwa tenga ambaye aljeruhiwa vbaya sana goti na
baba yangu mkubwa Kitwana Manara ‘Popat’.
Ifahamike hyo ilikuwa
mechi ya mechi ya marudiano dhidi ya Maafrica Magharibi hao ambapo kwenye game
ya kwanza kule Surulele Stadium Nigeria tulitoka suluhu bin suluhu.
Bahati mbaya kwetu
wakatufunga mbili mtungi huku ikitajwa kukosekana kwa tenga kuliififisha
defence line ya Stars. Siku hiyo alitumika defender chipukizi(wakati huo) Chukwu
ambaye ndiye aliyeziba pengo la captain Tenga
Iwapo kama
tungefanikiwa kuwatoa wala pilipili wale. Stars ilikuwa ikutane na Algeria
ambao ndio waliofuzu kucheza Kombe la Dunia la Spain 1982,
Mungu jalia bahati
haikuwa yetu. Lakini tulikuwa karibu kabisa na World Cup kuliko kipindi chochote
cha uhai wa taifa hili!
Katika miaka yake yote
ya uhai wa mataifa yetu mawili. Nchi hizi zmekutana mara tatu tu. Ukiacha game
hizo za kufuzu kwa Kombe la Dunia. Stars na mwewe hawa washawahi kukutana pia
kwenye mechi ya ufunguzi wa Kombe la Mataifa huru ya Africa (Afcon) pale Lagos
na Stars tukalala 3-1.
Miaka ya mwishon mwa miaka
ya 1990 tulicheza nao lakini ilikuwa kwenye mechi ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki
ambayo wachezaji wanaoruhisiwa kucheza ni wale walio chini ya miaka 23.
Mechi hizi pia wapo
hao walitutoa na nakumbuka walikuja na nyota wao Tijan Babangida ambaye ni
ndugu wa winga mahiri wa zamani wa ajax Amsterdam.
Nimeandika waraka huu
mrefu kdogo ili itukumbushe shughuli tuliyo nayo mbeleni. Kwanza kihistoria
baina yetu, pili kiuhalisia kuhusu uwezo wa kabumbu wa wapinzani wetu hawa
ambao wamejaaliwa mamia ya wanasoka wanaocheza soka huko Ulaya.
Najua kwenye mpira
lolote linawezekana. But tuendelee na maandalizi yetu huku tukiomba kwa Mungu
pia, na hasa kheri tunaweza kuishangaza Afrika kwa kuwafunga manguli hawa wa
kandanda si Afrika tu bali ulimwenguni kote.
Nimalizie kwa kuwataka
radhi kwa errors mbili tatu.na kuwaomba sote kwa pamoja tuweke silaha chini kwa
interest ya taifa letu
Mungu ibariki Stars
Mungu ibariki Tanzania
Amiin
Haji S.Manara
0 COMMENTS:
Post a Comment