Ikiwa ndiyo mechi yake
ya kwanza ya Ligi Kuu England akiwa na Man City, Raheem Sterling ameonekana
tayari kuwa kipenzi cha mashabiki.
Sterling ambaye
amejiunga na Man City akitokea Liverpool kwa dau la pauni milioni 49,
aliichezea Man City katika mechi dhidi ya Wes Brom.
City waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na Sterling alichukua jezi yake na kuigawa kwa mtoto wa kike aliyekuwa jukwaani.
Licha ya walinzi
kumsisitiza wakimtaka kutokwenda kwenye eneo hilo la mashabiki, lakini alifanya
hivyo hadi akamkabidhi hezi hiyo aliyetaka kumpa.
0 COMMENTS:
Post a Comment