August 8, 2015

AWADHI JUMA AKISHANGILIA NA WENZAKE MARA TU BAADA YA KUCHEKA NA NYAVU...
Unakumbuka miaka mitatu iliyopita, yote mfululizo Simba ilikuwa ikipoteza mechi zake katika Simba Day, basi si mwaka huu!

Maana Simba imefuta uteja wa Simba Day ambayo ni siku yake maalum baada ya kuichapa SC Villa ya Uganda kwa bao 1-0.
 
Katika mechi hiyo tamu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo, Simba ililazimika kusubiri hadi dakika za jioni kupata bao hilo kupitia kwa Awadhi Juma aliyeingia kipindi cha pili.
SC Villa nao walionyesha wako vizuri kwa kuipa shida kubwa Simba ingawa kiungo cha Mwinyi Kazimoto na Said Ndemla kilikuwa kimepikika.

Kabla ya hapo wachezaji walitambulishwa pamoja na benchi la ufundi huku kukiwa na mechi mbili za utangulizi ambazo zilikuwa burudaaani ile mbaya.

HATIMAYE MO DEWJI AMEREJEA UWANJA WA TAIFA TENA...






UKAWA KAMA KAWA.....

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic