Katibu Mkuu wa zamani wa TFF,
Frederick Mwakalebela, leo alitoa kali pale alipoamua kupiga push up maarufu
kama Magufulika.
Upigaji push up umekuwa ukiitwa
Magufulika kutokana na mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), John
Magufuli kupenda kuutumia.
Mwakalebela ambaye anagombea ubunge
wa Iringa mjini kupitia CCM, aliamua kufanya push up na kushangiliwa sana na
Wana-CCM waliokuwa wamejitokeza kwa wingi sana.
Hata hivyo kutokana na kuchoka sana,
Mwakalebela alilazimika kuinuliwa na msanii wa Hip Hop, Hamis Mwinjuma maarufu
kama MwanaFA ambaye ‘WaliMagufulika’ pamoja, lakini mwenzake akaonekana kuwa
fiti zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment