| FARID ALIYEIPA AZAM USHINDI |
Mabao mawili ya Kipre Tchetche na Farid Mussa yameipa Azam FC mwanzo mzuri wa Ligi Kuu Bara.
Azam FC ikiwa nyumbani Chamazi imeibuka na ushindi wa mabao hayo 2-1 dhidi ya Prisons ya Mbeya ambayo ilionekana kukomaa.
Licha ya Azam kuanza kufunga bao kupitia kwa Kipre, lakini Prisons walisawazisha kabla ya kinda Farid ambaye yuko kwenye kikosi cha Stars kufunga bao la pili.
Prisons ambao wamesafiri kutoka Mbeya, wameondoka mikono mitupu zaidi ya kupata bao hilo moja.







0 COMMENTS:
Post a Comment