September 12, 2015

KIIZA
Simba imefanikiwa kuanza vizuri Ligi Kuu Bara baada ya ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya African Sports ya Tanga.

Shukurani kwa Mganda Hamis Kiiza ambaye alifunga bao hilo pekee kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Angalau Simba, iliweza kuonyesha soka ala kuvutia katika kipindi cha pili tofauti na mambo yalivyokuwa katika kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili, Simba wangeweza kufunga mabao zaidi, lakini walishindwa kuwa makini walipofika kwenye lango la Wana Kimanukanu waliopanda daraja msimu huu

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic