Kocha wa JKT Ruvu, Fred
Felix Minziro, amebwaga manyanga.
Minziro anaondoka, mechi yake ya mwisho ikiwa ni dhidi ya Stand United waliolala kwa bao 1-0 lililofungwa na straika nyota wa zamani wa Simba, Elius Maguri.
Minziro ameachia ngazi
katika nafasi yake hiyo baada ya kuona mwenendo wa kikosi chake si mzuri katika
Ligi Kuu Bara.
Kocha huyo ameamua
kuachia ngazi saa chache baada ya JKT kupokea kipigo cha bao 1-0 dhid ya Stand
United tena JKT wakiwa nyumbani, jana.
Katibu Mkuu wa JKT, Ramadhani
Madoweka amesema kweli Minziro ameachia ngazi.
“Kweli Minziro ameachia
ngazi, timu sasa iko chini ya Greyson Haule,” alisema.
JKT iko njiani kwenda
mkoani Tabora ambako ina kibarua kingine kigumu dhidi ya Kagera Sugar ambayo
inatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.
Hadi Minziro anaondoka
alikuwa ameongoza timu hiyo katika mechi nne, akianza ugenini dhidi ya Majimaji
mjini Songea ambako walilala kwa bao 1-0.
Baada ya hapo, wakasafiri
kwenda Mbeya ambako walichapwa bao 3-0 na Prisons kabla ya kutua jijini Dar es
Salaam walipokutana na kipigo cha paka mwizi cha mabao 4-1 dhidi ya Yanga na
jana, wakiwa nyumbani kwa mara ya kwanza, wakadundwa 1-0 na Stand.
0 COMMENTS:
Post a Comment