Kiungo Mbrazil, Andre
Coutinho ameweka rekodi ya kukaa benchi kwa mechi nne mfululizo.
Coutinho amekaa nje mechi
ya nne mfululizo huku Yanga ikishinda mechi yake ya nne mfululizo.
Mechi zote nne, Coutinho
amekuwa akikaa benchi pamoja na beki Vicent Bossou raia wa Togo.
Mechi ya kwanza Yanga
iliifunga Coastal Union mabao 2-0, ikaishinda Prisons mabao 3-0 kabla ya
kuitwanga JKT Ruvu mabao 4-1.
Baada ya hapo, Yanga
imekutana na watani wake Simba na kuwashinda kwa mabao 2-0, Mbrazil huyo
aliendelea kuwa kwenye benchi.
0 COMMENTS:
Post a Comment