September 22, 2015


Kitabu kipya cha Kocha Sir Alex Ferguson kiitwacho Leading kina mambo aisee.


Kocha huyo ametoa kitabu hicho akisimulia mambo mengi sana wakati akiwa Kocha wa Manchester United na moja wapo ni wachezaji aliowahitaji lakini akawakosa na baadaye wakawa nyota duniani kote.


Amanza na mshambuliaji Ronaldo de Lima wa Brazil ambaye alimkosa, baadaye akatua PSV kabla ya kwenda Barcelona na baadaye akawa nyota duniani kote.

Pia alimzungumzia nyota wa Bayern Munich, Thomas Muller ambaye alimkosa akiwa na miaka 10.


Halafu akawataja nyota wawili wa Chelsea, baadaye. Je, unawajua? Hao ni kipa Petr Cech pamoja na mshambuliaji hatari aliyestaafu, Didier Drogba.
Anasema alimuona Drogba akiwa Marseille ya Ufaransa, klabu hiyo ikataka pauni milioni 25. Wakati wanaulizana wafanyeje, Chelsea wakawawahi.

Kwa upande wa Ronaldo, naye alikuwa tayari kujiunga wakati akicheza kwao, lakini suala la kibali cha kazi likawa tatizo, mwisho akaenda zake PSV.


Mwingine ni Sergio Aguero ambaye hadi makubaliano yalianza, lakini alilalama kwamba wakala wake alitibua kwa kutaja bei kubwa sana. Wakashindwa.

Lucas Moura, pia Ferguson akamtaka na wakawa tayari kutoa pauni milioni 24, lakini mamilionea wa Ufaransa, PSG wakaibuka na kuweka mezani pauni milioni 45.

Beki Raphael Varane ambaye sasa anakipiga Real Madrid pia alikuwa chaguo lake, wakakubaliana na mwisho Zinedine Zidane akaingilia na kumpeleka Madrid.
“Ilikuwa ni Zidane, nakumbuka wakati huo Mourinho ndiye alikuwa kocha wa Real Madrid. Lakini sidhani kama hata aliwahi kumuona akicheza hadi alipopelekwa na Zidane,” alisema.

WENGINE:
Ferguson aliwataja wachezaji wengine aliowahi kutaka kuwasajili lakini akawakosa kuwa ni washambuliaji hatari enzi hizo kama Alan Shearer pia Patrick Kluivert.


Kwa sababu tofauti, aliwakosa  Gabriel Omar Batistuta, Samir Nasri na Glenn Hysen.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic