Na Omary Katanga
RAIS wa Shirikisho la soka nchini (TFF),
Jamal Malinzi, amefunga kozi ya wiki mbili ya makocha lesseni C inayotambuliwa
na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) na kuwataka wahitimu hao kufanyia
kazi mafunzo waliyoyapata.
“Hiki mlichokipata kwenye mafunzo haya
mnatakiwa muende mkafanyie kazi kwa kutafuta timu za kufundisha na baada ya
mwaka mmoja ni vizuri mkajiendeleza zaidi ya hapa,” alisema Malinzi.
Aidha, amesema kuwa Shirikisho lake
limepanga kuhakikisha baada ya muda litafuta utaratibu wa makocha wenye lesseni
C kuwa kwenye benchi la ufundi la timu za daraja la kwanza na kuwa wasaidizi
kwenye benchi la ufundi la timu za ligi kuu.
“kwa sasa hivi makocha wa ligi kuu
wanatakiwa kuwa na leseni ya daraja B na wasaidizi angalau leseni daraja C, ila
kuanzia msimu wa 2017-2018 mambo yatabadilika na leseni C aizataruhusiwa
kwenye mabenchi ya ufunzi kwa timu za ligi kuu, mambo yataendelea hivyo mpaka
mwisho tutakuwa na leseni za daraja A,” alisema Malinzi.
Aidha, aliwataka wahitimu hao ambao wengi
wao wanatoka kwenye klabu za daraja la kwanza na wengine wakiwa makocha
wasaidizi kwenye klabu za ligi kuu, kuhakikisha wanatumia ujuzi walioupata
kwenye mafunzo hayo kuzisaidia timu zao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha
soka mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo, ameishukuru TFF kwa jitihada za
kuendeleza mchezo wa soka nchini na kuelelezea changamoto wanazokutana nazo
katika kuandaa kozi kama hizo kwa vyama vya soka vya mikoa nchini.
“Sisi DRFA tumefanikiwa kuendesha kozi hii
kwa sababu ya uwepo wa timu za Simba, Yanga na Azam kwenye ligi kuu ambazo ni
sehemu ya mapato kwa chama chetu, ila kwa vyama vingine hali inakuwa ngumu
kuandaa na kuendesha mafunzo kama hayo,” alisema Kasongo.
Kozi hiyo ya wiki mbili ilikuwa ikifanyika
kwenye ukumbi wa TFF na kuendeshwa na mkufunzi anayetambulika na Caf, Salum
Madadi ambaye pia ni Mkurugenzi wa ufundi wa TFF.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA SOKA MKOA WA
DAR ES SALAAM –DRFA








0 COMMENTS:
Post a Comment