Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema asingeweza kuinywa supu ya mawe
waliyowaandalia Yanga, badala yake wameshituka.
Hans Poppe amesema
wasingeweza kuinywa supu hiyo kwa kuwa ilikuwa ya Yanga. Hivyo Yanga hawapaswi
kuiga ila waseme waliiangalia Simba kitu gani.
“Waache kuiga, sisi tulisema tokea mapema kwamba tuliwaangalia supu ya mawe. Sasa nao waseme walituandalia nini.
“Mimi naona wana haki ya
kuitema, maana wameinywa kwa miaka minne mfululizo. Sasa wana haki ya kuitema,”
alisema.
Yanga imeichapa Simba kwa
mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam, jana.
0 COMMENTS:
Post a Comment