September 27, 2015



Kikosi cha Azam FC kimeendeleza ushindi katika Ligi Kuu Bara baada ya kushinda kwa maba 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.


Azam ilianza Ligi Kuu Bara kwa kuichaa Prisons bao 2-1, ikaendeleza kipigo cha 2-0 kwa Stand United kabla ya kuitandika Mwadui FC 1-0.

Sasa ina pointi 12 sawa na Yanga na Mtibwa Sugar ambazo hazijapoteza hata mechi moja katika nne zilizocheza.

Mabao ya Azam FC katika mchezo huo yalifungwa na kiungo Mudathir Yahya katika dakika ya 11 kabla ya Kipre Tchetche kumaliza kazi katika dakika ya 52.

Hata hivyo, Mbeya City walijitutumua na kupata bao katika dakika ya 55 kupitia kiungo wao Raphael Alpha.

Hata hivyo, dakika za mwisho Mbeya City walionekana kukaa vizuri zaidi na kuwahenyesha Azam FC ambao hata hivyo safu yao ya ulinzi ikiongozwa na Serge Wawa ilionekana kusimama imara.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic